Hamas iko tayari kutekeleza matakwa ya mpango wa Biden
16 Juni 2024Akizungumza hii leo Haniyeh ameweka wazi kwamba kundi hilo na makundi mengine ya Wapalestina yako tayari kufanikisha pendekezo hilo linalojumuisha, kusitishwa kwa mapigano, kuondoka kwa wanajeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza, kujengwa upya kwa mali iliyoharibiwa na makubaliano makubwa ya kubadilishana wafungwa pamoja na mateka wanaoendelea kuzuiliwa na kundi hilo la Hamas.
Vita kati ya Israel na Hamas vimeingia mwezi wa saba
Tarehe 31 mwezi Mei, Biden alitangaza mpango wa awamu tatu ya pendekezo la Israel, lililojumuisha majadiliano ya kusitisha mapigano kikamilifu Gaza na kuachiwa kwa mateka wa Israel ili nao wafungwa wa Kipalestina waweze kuachiwa huru.
Kando na kauli hiyo Israel na Hamas wameendelea kukataa vipengee muhimu katika mpango huo.