Islamic Jihad watangaza kusitisha mashambulizi Gaza
3 Mei 2023Matangazo
Wapatanishi kutoka Qatar, Misri na Umoja wa Mataifa waliingilia kati kurejesha utulivu kuanzia majira ya saa 10 alfajiri kwa saa za Mashariki ya Kati. Msemaji wa Islamic Jihad, Tariq Salmi amesema awamu moja ya mapambano imemalizika, lakini maandamano ya upinzani yataendelea.
Salmi amesema wapiganaji wao jasiri wameonesha uaminifu na kujitolea kuwatetea watu wao. Khader Adnan aliyegoma kula kwa takribani miezi mitatu alifariki jana akiwa chini ya ulinzi wa Israel.
Kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh ameitaka Israel kuurejesha mwili wa Adnan kwa familia yake.