ISLAMABAD:Majeshi ya NATO yataka askari zaidi kupambana na Wataleban huko Afghanistan
22 Januari 2007Kamanda wa majeshi ya NATO huko Afghanistan, General David Richards amesema kuwa anahitaji askari na fedha zaidi kwa mwaka mmoja zaidi ili ili kuwasambaratisha wanamgambo wa kitalaban.
Mkuu huyo wa majeshi ya NATO huko Afghanstani amenukuliwa na gazeti la Guardian la Uingereza akisema kuwa itakuwa ni hisia za hatari kufikiria kuwa hali ilivyokuwa mwaka jana itakuwa vivyo hivyo mwaka huu.
Amesema kuwa si tu hatua za kijeshi zinahitajika, bali juhudi zaidi kuwawezesha raia kuongeza kasi na uwezo wa kuijenga nchi yao.
Nchini Pakistan bomu lililotegwa pembeni ya barabara limewaua askari watatu wa Pakistan katika mji wa kaskazini magharibi katika mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.
Maafisa wamesema kuwa shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Miranshah ambao ni mji mkuu wa jimbo la Waziristan, ambako ni ngome ya wanaunga mkono wataliban.
Mwaka jana Serikali ya Pakistan, ilitiliana na saini mkataba wa amani kumaliza machafuko na wazee wa kikabila wa eneo hilo.