1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD. Watuhumiwa zaidi wa al-Qaeda wakamatwa nchini Pakistan.

5 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGM

Walinda usalama nchini Pakistan wamewatia mbaroni watu wengine zaidi wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la al-qaeda. Watu hao wamekamatwa wakati wa misako iliyofanywa nchini kote, kufuatia kuhojiwa kwa Abu Faraj al Libbi, ambaye alikamatwa hapo awali.

Libbi anachukua nafasi ya tatu ya maongozi ya kundi hilo la al-qaeda, na anakabiliwa na mashtaka ya kupanga njama ya kutaka kumuua rais wa Pakistan, Pervez Musharaf miezi 18 iliyopita. Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo alithibitisha kukamatwa kwa Libbi, akisema mtuhumiwa huyo anaongoza operesheni za kundi la al-qaeda ulimwenguni kote.

Watu 17 waliuwawa katika majaribio mawili ya kutaka kumuua rais Musharaf mwezi Disemba mwaka wa 2003.