1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Wabunge wamchaguwa rais leo

Mohamed Dahman6 Oktoba 2007

Wabunge wa bunge la taifa na wa majimbo wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais nchini Pakistan.

https://p.dw.com/p/C7iT
Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan.
Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan.Picha: picture-alliance/dpa

Rais Generali Pervez Musharraf anatagemewa kushinda kipindi kengine cha miaka mitano madarakani juu ya kwamba bado hakuna uhakika iwapo Mahkama Kuu itaidhinisha uamuzi huo kwa vile mshindi hatotangazwa hadi hapo mahkama hiyo itakapotowa hukumu iwapo Musharraf anaweza kushika madaraka wakati bado akiwa kiongozi wa kijeshi.

Musharraf ameahidi kun’gatuka jeshini iwapo atachaguliwa tena na kuapishwa kushika wadhifa wa urais akiwa kiongozi wa kiraia miaka minane baada ya kuingia madarakani kwa mapinduzi. Zaidi ya wabunge 180 wa muungano wa upinzani unaoongozwa na Nawaz Sharif wamejiuzulu kupinga uchaguzi huo.

Chama cha Wananchi wa Pakistan PPP hakitosusia uchaguzi huu kufuatia Musharraf kufuta mashtaka ya rushwa dhidi ya kiongozi wake Benazir Bhutto kutokana na makubaliano ya kushirikiana madaraka.