1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Viongozi wa Asia kujadili usalama

4 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFmK
Viongozi wa nchi za kusini mwa Asia wanakutana katika kikao cha siku 3 mjini Islamabad ambacho lengo lake ni kukuza ushirikiano wa biashara na kuimarisha usalama wa eneo hilo. Mkutano huo wa viongozi wa nchi 7 za Jumuia ya Ushirikiano wa SAARC ni wa kwanza kufanyika katika muda wa zaidi ya miaka 2. Mapendekezo ya mkataba wa ushirikiano wa kibiashara yalikamilishwa katika kikao cha mawaziri kilichomalizika hapo jana. Mkutano huo umekuwa pia fursa ya kwanza kwa Waziri mkuu wa India, Atal Behari VAJPAYEE kuizuru Pakistan katika miaka mitano. Kiongozi huyo ametaja kuwa India inakusudia kutumia nafasi hiyo kwa majadiliano zaidi na Pakistan kuhusu mzozo wa jadi kati ya nchi hizo 2 kubwa za Bara Hindi kuhusu mamlaka ya jimbo la mpakani la Kashmir. Haijulikani hata hivyo kuwa Bwana VAJPAYEE atafanya mazungumzo ya binafsi na Rais wa Pakistan, Pervez MUSHARRAF. Imeripotiwa hata hivyo kuwa Waziri mkuu wa India ameanza mazungumzo na mwenzie wa Pakistan Zafarullah JAMALI mara baada ya kikao hicho cha wakuu wa nchi na serikali wa Jumuia hiyo ya Asia.