ISLAMABAD: Kombora laweza kupachikwa silaha za nyuklia
31 Machi 2007Matangazo
Pakistan imefanikiwa kujaribu kombora la masafa mafupi likiwa na uwezo wa kubeba silaha ya kinyuklia.Kwa mujibu wa jeshi la Pakistan,kombora “Abdali” lina uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 200 na linaweza kupachikwa kila aina ya silaha. Hilo ni jeribio la pili kufanywa na Pakistan tangu juma lililopita.Pakistan na jirani India mara kwa mara hufanya majeribio ya makombora, kufuatia yale majeribio ya kinyuklia ya mwaka 1998.