1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Kiongozi wa Wataliban Mollah Omar atishia kwa mashambulizi zaidi dhidi ya majeshsi ya NATO

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD01

Kiongozi wa wapiganaji wa kitalibani Mullah Mohammad Omar ameyataka majeshi ya kambi ya kujihami ya nchi za magharibi NATO kuondoka kutoka Afghanistan na kutishia juu ya mashambulizi makali zaidi wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ukimalizika. Katika ujumbe wake uliotangazwa na shirika la habari lenye makao yake nchini Pakistan, kiongozi wa kitalibani ametishia kumfikisha rais wa Afghanistan Hamid Karzai mbele ya mahakama ya kiislamu.

Mollah Omar anajificha tangu mwaka wa 2001 ulipopinduliwa utawala wa kitalibani na majeshi ya kigeni yakiongozwa na Marekani.

Kwa upande mwingine, Italy imesema muda wa mwisho uliowekwa na watekaji nyara wa mwandishi mpigapicha wa kitaliyani Gabrielle Torsello umepita. Mwandishi huyo wa habari alikamatwa siku 10 zilizopita kusini mwa Afghanistan.

Watekaji nyara wanaitaka Italy kuyaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan.

Wakti huo huo, Umoja wa mataifa unasema milioni 43 za $ za kimarekani zinahitajika kwa ajili ya misaada ya chakula kwa raia wa Afghanistan kabla ya kuingia kipindi kigumu cha baridi.