1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Kauli ya Musharraf kuhusu ubakaji yashutumiwa

16 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaV

Hasira imechemka nchini Pakistan na nchi za nje leo hii kufuatia tamko la Rais Pervez Musharraf wa Pakistan kwamba Wapakistani wengi wanahisi kulia kuwa umebakwa ni njia rahisi ya kujipatia fedha na kuhamia Canada.

Waziri Mkuu wa Canada Paul Martin tayari alikuwa amelaani matamshi hayo yaliotolewa na Musharraf ambaye alikuwako Marekani kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo Jumaatano.

Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Kimataifa la Amnesty lenye makao yake mjini London Uingereza limesema Musharraf anapaswa kuomba radhi na magazeti nchini mwake pia yamelaumu msimamo huo wa kiongozi wao.

Musharraf ameliambia gazeti la Washington Post katika mahojiano hapo Jumanne kwamba Pakistan haipaswi kutajwa pekee yake katika masuala ya ubakaji kwa vile nchi nyengine zina matatizo kama hayo.

Gazeti hilo limemkariri Musharraf akisema kwamba lazima watu wafahamu mazingira ya Paskitan kwamba suala hilo limekuja kuwa la kijitafuatia fedha na kwamba watu wengi wanasema iwapo unataka kwenda nchi za nje na kupata visa au uraia na kuwa bilionare tajiri mkubwa kabisa nenda ukajibakishe.