Islamabad. Fedha za misaada hazijafika.
26 Oktoba 2005Matangazo
Licha ya miito kadha ya dharura, umoja wa mataifa umepokea pungufu ya theluthi moja ya fedha inazozihitaji kwa ajili ya misaada wa watu walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Pakistan.
Taasisi hiyo inasema kuwa siku 16 baada ya tetemeko la ardhi katika eneo la Kashmir, mataifa wanachama yametuma kiasi cha dola milioni 90 tu kati ya dola milioni 312 zinazohitajiwa.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ameziomba serikali kufika katika mkutano mjini Geneva leo Jumatano ili kupanga mipango ya misaada kwa ajili ya watu milioni tatu ambao wamekimbia makaazi yao kutokana na tetemeko hilo la ardhi.