1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ireland kujadili bajeti ya kubana matumizi

Kabogo Grace Patricia23 Novemba 2010

Hali hiyo inatokana na Ireland kutaka kubana matumizi ili iweze kupatiwa mkopo wa mabilioni ya Euro kutoka kwa Umoja wa Ulaya na IMF wa kukabiliana na mzozo wake wa kifedha.

https://p.dw.com/p/QFha
Waziri Mkuu wa Ireland, Brian Cowen.Picha: AP

Ireland leo inapanga kuanza wiki mbili za mabishano ya kisiasa wakati serikali ikibaliwa na upinzani wa kuzuia bajeti ya kubana matumizi ambayo inatokana na mkopo wa mabilioni ya Euro utakaotolewa na Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF.

Waziri Mkuu wa Ireland Brian Cowen, jana alilipuuzia shinikizo linaloendelea la kumtaka ajiuzulu akisema kuwa ataendelea kubakia ofisini hadi hapo bunge litakapoipitisha bajeti hiyo.

Amesema ataitisha uchaguzi wa mapema. Serikali inatarajia kutangaza kupunguza matumizi katika kima cha chini cha mshahara pamoja na matumizi ya huduma za kijamii.

Pia inatarajia kupunguza idadi ya wafanyakazi wa umma na kuongeza kodi ya mali mpya na kodi ya mapato.

Mageuzi yote hayo yanakusudia kupunguza Euro bilioni 6 kutoka bajeti ya mwaka ujao na Euro bilioni 15 kutoka katika bajeti ya kila mwaka ifikapo mwaka 2014.