Iraq yawasaka walioiba $2.5 billioni
4 Machi 2023Taarifa hiyo ilitolewa siku ya Jumamosi (Machi 4) na mamlaka ya kupambana na ufisadi nchini Iraq ambayo imeutaja wizi huo kama moja ya kashfa kubwa zaidi za ufisadi kuwahi kutokea nchini humo.
Afisa mmoja wa katika mamlaka hiyo, ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema watu hao ni pamoja na waziri wa zamani wa fedha na ndugu wa waziri mkuu wa zamani, Mustafa al-Kadhemi, ambaye anaishi nje ya nchi.
Soma zaidi: Wafuasi wa Sadr waondoka majengo ya serikali
Kundi la ulamaa mwenye usemi mkubwa Iraq al Sadr latwaa ushindi
Kwa mujibu wa afisa huyo, watu hao ni waziri wa zamani wa fedha, Ali Allawi, aliyekuwa mkurugenzi wa baraza la mawaziri, Raed Jouhi, katibu wake, Ahmed Najati, pamoja na mshauri wake, Mushikir Abbas.
Fedha hizo ziliibwa kati ya Septemba 2021 na Agosti 2022.