1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IRAN YATUHUMIWA NA IAEA:

12 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEEQ
VIENNA: Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia shughuli za atomiki IAEA,limeituhumu Iran kuwa ilikuwa na harakati za kinyuklia tangu miaka 20 iliyopita.Miongoni mwa shughuli hizo kulisafishwa pia madini ya plutonium,ingawa hadi hivi sasa hakuna ushahidi kuwa nchi hiyo inajaribu kutengeneza bomu la atomiki.Marekani inaituhumu Iran kuwa kwa siri inajaribu kutengeneza silaha za kinyuklia kwa kuutumia mpango wake wa kinyuklia kupata nishati.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa shughuli zake za kinyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya kiraia.