Iran yatetea haki ya kuendelea na mradi wake wa nyuklia
1 Desemba 2007Iran haiwezi kulaumiwa kuhusu masikitiko ya Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana kufuatia mkutano wa London juu ya mradi wa nyuklia wa Iran.Solana siku ya Ijumaa alisema kuwa amevunjika moyo baada ya mazungumzo ya mjini London kushindwa kusonga mbele.
Saeed Jalili alie msuluhishi wa Iran katika majadiliano ya mgogoro huo amesema,ukweli ni kwamba Iran imetetea haki yake na kusisitiza utekelezaji wa wajibu wake.Amesema, ran haipo tayari kukubali cho chote kilicho zaidi ya matakwa ya Mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia.
Mara kwa mara Iran imessema kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.Lakini Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi zina wasi wasi kuwa Iran inapanga kutengeneza silaha za nyuklia.Kwa upande mwingine,nchi tano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani zinakutana hii leo katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris kuzingatia kuiwekea Iran vikwazo zaidi kuhusika na mradi wake wa nyuklia.