1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema itaunga mkono mazungumzo ya amani Lebanon

15 Novemba 2024

Iran itaunga mkono uamuzi wowote utakaochukuliwa na serikali ya Lebanon pamoja na kundi la Hezbollah katika mazungumzo ya sasa ya kusitisha mapigano.

https://p.dw.com/p/4n3W7
Ali Larijani, mshauri mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei,
Ali Larijani, mshauri mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei.Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Hayo yamesemwa hivi leo na Ali Larijani, mshauri mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, amesisitiza kuwa Tehran haina nia ya kuhujumu mazungumzo hayo.

"Hatuna nia ya kuvuruga chochote. Tunalenga kuupatia suluhisho mzozo uliopo. Kwa hali yoyote ile, tunasimama na watu wa Lebanon na kuwaunga mkono. Wanaoleta usumbufu ni Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na washirika wake. Tujaribu kuwatambua marafiki na maadui zetu.”

Larijani alikutana kwa mazungumzo mjini Beirut na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati pamoja na Spika wa Bunge Nabih Berri, huku akisisitiza kuwa Iran itaendelea kuliunga mkono kundi la Hezbollah.