1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yapinga mahusiano kati ya Israel na mataifa ya kiarabu

1 Oktoba 2023

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amekosoa juhudi zote za mataifa ya kanda ya Mashariki ya Kati na eneo la Ghuba za kuimarisha mahusiano yao na Israel, taifa ambalo ni hasimu mkubwa wa serikali ya Tehran.

https://p.dw.com/p/4X1Km
Rais Ebhahim Raisi wa Iran
Rais Ebhahim Raisi wa IranPicha: Iran's Presidency/Mohammad Javad Ostad/WANA/REUTERS

Akihutubia Kongamano la Kimataifa la Mshikamano wa Kiislamu linalofanyika mjini Tehran, kiongozi huyo wa Iran amesema kusawazisha mahusiano na Israel ni ishara ya "kupotoka" kwa serikali yoyote kwenye ulimwengu wa kiislamu.

Matamshi yake yanafuatia juhudi zinazoongozwa na Marekani za kufanikisha kupatikana mkataba wa kuanzisha mahusiano rasmi kati ya Israel na Saudi Arabia.

Mnamo siku ya Ijumaa, Marekani ilisema nchi hizo mbili zimepiga hatua kuelekea kufikiwa mkataba utakaomaliza uhasama wa miongo mingi.

Iwapo makubaliano hayo yatapatikana yatakuwa ni mwendelezo wa Israel kurekebisha mahusiano yake na nchi za Kiarabu ikiwemo yale yaliyotangulia kati ya nchi hiyo na mataifa matatu ya kiarabu.