Mpinazani Jamshid ashikiliwa nchini Iran
2 Agosti 2020Taarifa ya wizara ya usalama iliyonukuliwa katika televisheni ya umma, haijasema kwa jinsi gani, wapi au lini kuzuiliwa huko kulianza kufanyika. Taarifa hiyo imesema Jamshid Sharmahad alipanga na kuongoza shambulizi la kwenye kituo cha kidini katika mji wa kusini wa Shiraz. Watu14 waliuawa na wengine 215 walijeruhiwa.
Mtuhumiwa Jamshid Sharmahd anatambuliwa kama nani katika siasa za Iran?
Jamshid Sharmahd anatajwa kuwa ni kiongozi wa kundi la kigaidi, ambae aliongoza kundi la wenye kujihami kwa silaha na matukio ya kigaidi nchini Iran, (Tonder) akitokea Marekani. Taarifa ya Iran inamwelezea mtu huyo ambae ameshiriki operesheni ngumu kuwa katika kipindi hiki yupo katika mikono yenye nguvu za kumdhibiti.
Televishini ya Iran imeonesha vidio ya mtu anaejitambulisha kwamba ni Sharmhad na kutaja tarehe yake ya kuzaliwa. Mtu huyo baadae alioneshwa kwa kuzibwa macho akisema "Walitaka vilipuzi na tuwapa."
Hata hivyo kundi alikokuwa akiliongoza la Tondar halijathibitisha tukilo la kushikiliwa huko. Katika kile kinachoonekana kujibu ripoti ya kutekwa kwa Sharmhad, kundi hilo limesema katika tovuti yake halijathibitisha habari ambazo zimekuwa zikielezwa katika mitandao mbalimbali. Lakini hata hivyo katika taarifa yake ya awali kundi hilo lilisema litaendelea na mapambano hata kama halitakuwa na kiongozi wake.
Harakati la kundi la Tondar, likiongozwa kutoka Los Angeles
Likiwa na maskani yake mjini Los Angeles, Marekani kundi la Tondar linasema linapigania utawala wa kifalme wa Iran, ambao uliondolewa na mapinduzi ya Kiislamu ya 1979. Likiwa nje ya mipaka ya Iran, linaendesha radio ya kuegemea upande wa upinzani na televisheni.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema ina taarifa ya taarifa ya kuwekwa kizuizini kwa Sharmhad. Na kuongeza kuwa serikali ya Iran ina historia ndefu ya kuwaweka kizuizini Wairan na raia wa kigeni kwa mashitaka ya kubambikizwa. na hivyo kulitaka taifa hilo kuwa na uwazi na kujifungamanisha na sheria za kimataifa.
Soma zaidi:Iran yazindua makombora ya chini ya ardhini
Kwa mujibu wa tovuti ya kundi hilo la Tondar, Sharmhad ni Muiran/Mjerumani, mhandisi umeme ambae alizaliwa 1955 na kuishi Ujerumani kabla hajahamia Loss Angeles 2003. Hata hivyo wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani haijasema lolote.
Chanzo/: RTRE