1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yalaani vikwazo vya umoja ulaya na Uingereza

24 Januari 2023

Iran imelaani vikali vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Ulaya na Uingereza. Imesema itachukua hatua za kulipiza kisasi baada ya nchi za Magharibi kuiwekea mbinyo kuhusiana na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji.

https://p.dw.com/p/4McZq
Sprecher des iranischen Außenministeriums Naser Kanaani
Picha: jamaran

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran Nasser Kanaani amesema katika taarifa kuwa Iran itatangaza hivi karibuni orodha ya vikwazo vipya dhidi ya wakiukaji wa haki za binaadamu wa Umoja wa Ulaya na Uingereza.

Umoja wa Ulaya ulitangaza vikwazo dhidi ya zaidi ya maafisa 30 wa Iran na mashirika, vikiwemo vitengo vya kikosi cha ulinzi wa mapinduzi cha Iran, ukikilaumu kwa ukandamizaji wa kikatili dhidi ya waandamanaji na ukiukaji mwingine wa haki za binaadamu.

Marekani na Uingereza pia ziliiwekea Iran vikwazo vipya, kudhihirisha kudorora kwa mahusiano ambayo tayari ni mabaya mno kati ya nchi za Magharibi na Iran.