1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yaituhumu Israel kuhujumu mradi wake wa makombora

31 Agosti 2023

Iran imeituhumu Israel kwamba inajaribu kuhujumu mradi wake wa makombora ya masafa marefu kwa kupenyeza vipuri vya kigeni vyenye hitilafu na vinavyoweza kuripuka,kuharibika au kuharibu silaha hizo kabla ya kutumika.

https://p.dw.com/p/4Voqr
Iran Teheran | Iran Teheran | Leiter der AEOI Mohammed Eslami
Picha: Atomic Energy Organization Of Ir/ZUMA/picture alliance

Iran imetowa tuhuma kwamba mawakala wa shirika la ujaasusi la Israel Mossad,ndio wanaosambaza vipuri hivyo.

Israel haikutoa tamko mara moja kujibu tuhuma hizo zilizotolewa kupitia kituo cha  Televisheni cha serikali ya  Iran. 

Ripoti ya Iran imeitaja operesheni hiyo inayodai ni ya Israel,kuwa ni moja ya majaribio makubwa  ya hujuma ambayo haijawahi kuyaona.

Soma pia:Iran: Mashambulizi dhidi ya Syria huenda yakachochea visasi

Israel imekuwa ikishukiwa katika msururu wa mashambulio ya mauaji ndani ya Iran na baadhi ya hujuma za mashambulio hayo zimeharibu maeneo ya vinu vya Nyuklia ya Iran. 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW