Iran na madini ya Uranium.
24 Mei 2010Matangazo
Barua iliyosainiwa na Mkuu wa programu ya
nyuklia ya Iran, Ali Akbar Salehi,
imekabidhiwa kwa Mkuu wa Shirika la
Kimataifa la Nguvu za Atomic -IAEA- Yukiya
Amano katika mkutano uliodumu takriban
dakika 45 mjini Vienna, Austria.
Televisheni ya Taifa ya Iran imenukuu barua
hiyo kwa kusema kuwa makubaliano hayo ni
hatua kubwa kuweza kumaliza hofu juu ya
mpango huo.
Vyombo vya habari nchini Iran vimesema pia
barua hiyo itakuwa mwanzo wa majadiliano
zaidi juu ya kubadilishw mafuta kupitia
kusainiwa kwa makubaliano.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika
hilo la Atomiki, Mkurugenzi mkuu ataipeleka
barua hiyo Marekani, Ufaransa na Urusi ili
nchi hizo ziweze kuizingatia.
Nchi hizo ni sehemu ya makubaliano
yaliyofikiwa awali chini ya mkuu wa zamani
wa shirika hilo la Atomiki, Mohamed
ElBaradei, yaliyofikiwa Oktoba mwaka jana,
lakini hayakufanikiwa kufuatia matakwa ya
Iran kufanyike marekebisho.
Pendekezo hilo juu ya kubadilisha madini ya
uranium yaliyorutubishwa kwa kiwango cha
chini -LEU- kwa mafuta kwa ajili ya kuweza
kuendesha maabara ya Iran ya utafiti wa
matibabu, ambalo linalenga kuondoa hofu
kwamba Iran inataka kujipatia madini hayo
kwa ajili ya silaha za nyuklia, lilifikiwa wiki
iliyopita na nchi hiyo pamoja na Uturuki na
Brazil.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Uturuki
na Brazil walitia saini makubaliano
yanayojumuisha Iran kutuma kiasi cha kilo
1,200 ya madini yake ya Uranium
kurutubishwa nchini Uturuki na baadaye
yarejeshwe nchini Iran kutumiwa katika
matumizi ya nishati.
Akizungumza awali kuhusiana na nchi yake
ilivyotayari kutoa ushirikiano na jumuia ya
kimataifa, Mkuu wa programu ya nyuklia ya
Iran, Ali Akbar Salehi. alisema katika nia yao
njema na kuonesha utayari wao wa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa
la nguvu za Atomiki, wamekubali kufanya
mabadilishano kufuatana na utaratibu ambao
ulishikiliwa na nchi za magharibi, nao ni
kukubali kukabidhi madini ya nchi hiyo
yasiyosafishwa kwa nchi ya tatu.
Hata hivyo, mataifa ya magharibi yanaona
makubaliano hayo yanalingana na yale
ambayo Iran ilijitoa miezi sita iliyopita.
Iran ilitishia kuacha kutekeleza mpango huo
iwapo itakumbwa na vikwazo vya Umoja wa
Mataifa vilivyozingatiwa kuchukuliwa mwezi
ujao.
Mwandishi: Halima Nyanza(Reuters)
Mhariri: Miraji Othman
Matangazo