1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Iran ndiyo iliyosababisha kifo cha Mahsa Amini

8 Machi 2024

Uchunguzi mmoja wa Umoja wa Mataifa umebaini kuwa utawala wa Iran ulihusika na "vurugu zilizotokea" zilizosababisha kifo cha Mahsa Amini mnamo Septemba 2022. Vurugu hizo zilichochea maandamano ya nchi nzima.

https://p.dw.com/p/4dIhn
Marekani | Maandamano Mahsa Amini
Picha ya Mahsa Amini ikiwa imeshikwa wakati wa maandamano ya kutaka mabadiliko ya utawala nchini Iran kufuatia kifo cha Amini.Picha: Cliff Owen/AP Photo/picture alliance

Ripoti ya awali ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa imebaini haya. Wachunguzi pia wamesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ilitumia nguvu zisizohitajika kuyazuia maandamano yaliyozuka baada ya kifo cha Amini. Maafisa wa usalama wa Iran wamelaumiwa kwa kuwanyanyasa kingono waliokamatwa katika maandamano hayo. Kamatakamata hiyo iliyodumu kwa mwezi mzima ilisababisha vifo vya watu 500 na watu 22,000 kukamatwa. Iran haijatoa tamko lolote kuhusiana na ripoti hiyo hata baada ya shirika la habari la Associated Press kuwasiliana nao kuhusiana na ripoti hiyo.