Mwandishi wa habari wa Iran, Maryam Lotfi atiwa mbaroni
3 Oktoba 2023Matangazo
Gazeti analofanyia kazi la Shargh limesema alikuwa ameenda katika Hospitali ya Fajr katika mji mkuu "kutayarisha ripoti ya habari kuhusu hali ya msichana huyo wa miaka 16 aliefikwa na hali ngumu kwenye treni ya chini ya ardhi" siku ya Jumapili.Mazingira ya tukio hilo hayako wazi hadi sasa, huku afisa mkuu akikana "uvumi" wa kutokea ugomvi na wafanyakazi wa treni ya chini ya ardhi.Mwezi Agosti vyombo vya habari vya Iran viliandika kuwa mamlaka ya Irani imewahoji au kuwakamata waandishi wa habari zaidi ya 90 tangu kuzuka kwa wimbi la maandamano nchini kote mwaka jana.