Irak yanyakua Kombe la Asia
29 Julai 2007Hapo kabla,kocha wa Irak,Jorvan Viera alisisitiza umuhimu wa mchezo huu kwa wachezaji wake na nchi yao katika wakati huu wa ghasia za kisiasa nchini Irak.Alisema:
„Huenda ikawa wataweza kuyakaweka kando matatizo ili waweze kucheza mpira na kuwafurahisha wenzao nyumbani na kuwapatia sababu ya kutabasamu.“
Kwa upande mwingine maafisa nchini Irak wamepiga marufuku magari kutembea barabarani katika mji mkuu Baghdad na miji ya Kirkuk,Nadjaf na Kerbala. Kwa mujibu wa msemaji wa kijeshi wa ngazi ya juu, hatua hiyo imechukuliwa ili kuzuia mashambulizi dhidi ya washabiki wa kandanda waliokuwa wakifurahia Iraq kuingia katika fainali ya Kombe la Asia dhidi ya Saudi Arabia katika mji mkuu wa Indonesia,Jakarta.
Mapema juma lililopita hadi watu 50 waliuawa na zaidi ya 100 wengine walijeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu ya gari yaliolenga washabiki waliokuwa wakisherehekea ushindi wa Irak,baada ya kuifunga Korea ya Kusini katika nusu fainali.