Irak yachunguza kupotea kwa raia wa Israel na Urusi
7 Julai 2023Matangazo
Katika mahojiano kwenye televisheni nchini humo, msemaji wa serikali Bassem al-Awadi amesema, serikali inafanya uchunguzi rasmi kuhusiana na kupotea kwa msomi huyo.
Afisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hapo juzi ililituhumu kundi la Kataeb Hezbollah kwa kumshikilia, ila kundi hilo lenye silaha na linaloungwa mkono na Iran lilisema halihusiki na kupotea kwake.
Afisi hiyo ya Waziri Mkuu wa Israel inasema Tsurkov ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamifu katika chuo cha Princeton hajulikani alipo huko Irak kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu sasa.
Anadaiwa kusafiri na kuelekea Irak kwa kutumia pasi yake ya usafiri ya Urusi kwa ajili ya kufanya utafiti kuhusiana na shahada yake ya uzamifu.