Mamlaka huru inayosimamia utendaji kazi wa polisi nchini Kenya, IPOA, imeanzisha uchunguzi wa visa vya dhulma zinazodaiwa kufanywa na maafisa wa polisi nchini humo. Matukio haya yanajiri siku chache baada ya polisi kuwauwa watu wanne katika kaunti ya Kajiado waliokuwa wakiandamana. Sikiliza ripoti ya Wakio Mbogho kutoka Nakuru.