1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

IPC: Sudan inahitaji hatua za haraka kuepusha janga la njaa

30 Machi 2024

Mamlaka ya kimataifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa chakula imeonya kwamba hatua za haraka zinahitajika nchini Sudan ili kuzuia vifo na janga la njaa.

https://p.dw.com/p/4eGVL
Mzozo nchini Sudan | Kambi ya Gedaref
Raia wa Sudan wakiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika Jimbo la Gadaref baada ya kulazimika kuuhama mji mkuu Khartoum kufuatia mapigano:20.03.2024Picha: -/AFP/Getty Images

Taasisi hiyo inayofahamika kama IPC ilibainisha mwezi Desemba katika ripoti yake kwamba karibu watu milioni 5 wapo hatarini kukabiliwa na janga la njaa nchini Sudan.

Awali, Marekani ilitahadharisha kuwa italishinikiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kupeleka msaada kutokea Chad, kwa watu wanaokabiliwa na njaa nchini Sudan.

Soma pia: Baraza la usalama lahimizwa lisaidie msaada upelekwe Sudan

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema pande zinazozozana zimevuruga operesheni za utoaji misaada.