IOM: Zaidi ya watu 60 wahofiwa kufa maji Cape Verde
17 Agosti 2023Msemaji wa shirika hilo Safa Msehli ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu 63 wanahofiwa kufa maji.
Amesemawalionusurika ni 38 miongoni mwao wakiwa watoto wanne wenye umri wa kati ya miaka 12 na 16. Polisi ya Cape Verde imesema boti hiyo ya uvuvi iliyotengenezwa kwa mbao ilipatikana siku ya Jumatatu katika Bahari ya Atlantiki, umbali wa kilomita 277 kutoka kisiwa cha Sal nchini humo.
Boti hiyo ilitoka Senegal mnamo Julai 10 ikiwa imebeba watu 101. Hayo yamesemwa na wizara ya mambo ya nje ya Senegal iliyowanukuu manusura wawili.
Soma pia:Zaidi ya wahamiaji 600 waokolewa Bahari ya Mediterania
Kati ya watu waliokuwemo ndani ya boti hiyo mmoja alitoka Guinea Bissau, na wengine wote walikuwa Wasenegali. Abdou Karim, afisa wa chama cha wavuvi CLPA ameliambia shirika la habari la AFP kwambainahofiwa watu ambao hawajulikani waliko, huenda wote wakawa wamekufa.