1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOC yakosoa uamuzi wa Ukraine kuwazuia wanamichezo wake

1 Aprili 2023

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC, imekosoa uamuzi wa Ukraine kutoruhusu wanamichezo wake kushiriki katika mashindano ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024 ikiwa itahusisha wanamichezo wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4Pagh
IOC debattiert mögliche Wiederzulassung Russlands
Picha: FABRICE COFFRINI/AFP/Getty Images

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC, imekosoa uamuzi wa Ukraine kutoruhusu wanamichezo wake kushiriki katika mashindano ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024 ikiwa itahusisha wanamichezo wa Urusi.

Waziri katika serikali ya Ukraine, Oleh Nemchinov, alitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa baada ya IOC kutoa mapendekezo siku ya Jumanne ya kurejea taratibu kwa wanamichezo wa Urusi na Belarus katika mashindano ya kimataifa.

Wanamichezo kutoka nchi hizo mbili walipigwa marufuku kushiriki mashindano mengi ya kimataifa tangu Machi mwaka uliopita kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Katika taarifa yake, IOC imesema iwapo uamuzi huo utatekelezwa, utawaumiza wanamichezo wa Ukraine na hautakuwa na athari yoyote katika vita ambavyo ulimwengu unataka vikomeshwe.