1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOC kuzungumza na waandalizi wa michezo kuhusu Corona

Deo Kaji Makomba
16 Machi 2020

Ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla ya kuanza kwa mashindano ya Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020 hapo Julai 24, maswali yamekuwa yakijitokeza endapo kama mashindano hayo yatafanyika au la.

https://p.dw.com/p/3ZWnJ
Schweiz Lausanne Olympische Ringe
Nembo ya Mashindano ya OlimpikiPicha: picture-alliance/KEYSTONE/J.-C. Bott

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, IOC, Jumanne tarehe 17.03.2020 inatarajia kuwa na mazungumzo na viongozi wa taasisi za kimataifa za michezo kufuatia mlipuko wa virusi hatari vya Corona vilivyoibuka na kuleta taharuki kubwa katika nchi mbalimbali duniani, chanzo cha karibu kutoka ndani ya shirikisho hilo kimezungumzia kuhusiana na suala hilo.

Aidha chanzo kingine cha habari kimesema kuwa, siku hiyo ya Jumanne ya tarehe 17.03.2020, IOC itafanya  pia mkutano na bodi ya watendaji wa shirikisho hilo kwa njia ya vidio, mkutano ambao hapo awali haukuwa umepangwa

Chanzo cha ndani cha IOC, kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa hakuna maamuzi yaliyotarajiwa kuelekea siku ya Jumanne kutoka kwa bodi tendaji ya kamati hiyo.

Ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla ya kuanza kwa mashindano ya Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020 hapo Julai 24, maswali yamekuwa yakijitokeza endapo kama mashindano hayo yatafanyika au la.

Homa inayosababishwa na virusi hatari vya Corona vilivyoibuka nchini China mwishoni mwa mwaka jana, hadi kufikia sasa vimeua zaidi ya watu 6,000 duniani kote na kuathiri watu wengine zaidi ya 160,000

Imevuruga ratiba mbalimbali za mashindano ya kimataifa ikiwemo kufutwa au kuhairishwa kwa hafla mbali mbali za michezo kama vile mashindano ya kutafuta tiketi ya kufuzu mashindano ya Olimpiki. Pia kumeibuka suala la iwapo mashindano hayo yanafaa kufutwa au kusogezwa mbele.

Ingawa Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe na waandaaji wa mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020 mara kwa mara wamesema kuwa mandalizi kuhusiana na michezo hiyo yanayotarajia kufanyika kama ilivyopangwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Kyodo, Waziri mkuu Abe, bunge la nchi hiyo Jumatatu tarehe 16.03.2020 kuwa, mashindano ya Olimpiki yanayotaraija kufanyika mjini Tokyo, yataiwakilisha dunia katika mapambano janga la virusi hatari vya Corona. 

Kulingana na mahojiano yaliyofanywa na mtandao wa habari wa Kyodo kwa njia ya simu, asilimia 69 ya raia wa Japan walijibu kwa kusema kuwa wana wasiwasi endapo kama Tokyo itakuwa na uwezo wa kuandaa mashindano hayo yenye kukusanaya watu wengi kama ilivyopangwa. Hata hivyo mtandao huo wa habri hakueleza bayana kuwa ni watu kiasi gani walioulizwa katika mahojiano hayo.

Corona imeathiri maandalizi ya mashindano ya Olimpiki

Japan Tokio | Internationales Olympisches Komitee | John Coates & Yoshiro Mori
Viongozi wa kamati ya Kimataifa ya Olimpiki John Coates na Yoshiro MoriPicha: picture-alliance/dpa/Maxppp/Kyodo

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, IOC, imehoji kuhusiana na ripoti iliyotolewa na shirika la utangazaji la Japan, NHK  kuhusu mazungumzo ya athari za virusi vya Corona yaliyotarajiwa kufanyika jumanne yalikuwa ni mojawapo ya mazungumzo na washika wadau.

IOC katika taarifa yake kwa shirika la habri la Reuters imeeleza kuwa tangu kuanza kuenea kwa hali hiyo wiki kadhaa zilizopita, Kamati hiyo ya michezo ya Olimpiki imekuwa ikitoa taarifa mara kwa mara kwa wadau juu ya taarifa mpya na kwamba simu ni sehemu ya mawasiliano ya mara kwa mara.

Mashindano kadhaa ya kufuzu katika michezo hiyo ikiwemo kukwea, ngumi, judo na mchezo wa kushindana kwa vitara au fencing katika kiingereza imeahirishwa au kusogezwa mbele na kuwacha wanariadha wakibaki mrama kuhusiana ni kwa jinsi gani na lini wataweza kufuzu katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2020 ya mjini Tokyo.

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 1,484 Jumapili iliyopita pamoja na 697 kutoka kwenye meli ya kifahari ya Dimond Princess na werngine 14 waliorudi na ndege za kukodi kutoka China. Vifo vilivyotokana na virusi vya Corona nchini Japan ni 29.