1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

​​​​​​​IOC kuamua dhidi ya Urusi

4 Desemba 2017

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki inakutana kesho kuamua kama itaizuia Urusi kushiriki katika Mashindano ya Olimpiki ya msimu wa Barafu mwaka wa 2018

https://p.dw.com/p/2ojzX
Sotschi 2014 - Team Russland mit Subkow
Picha: picture alliance/dpa/epa/B. Walton

Mnamo Novemba 26, shirikisho la riadha la kimataifa – IAAF lilishikilia marufuku yake ya miaka miwili dhidi ya Urusi kuhusiana na madai ya mpango wa serikali wa kufadhili matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku. Marufuku hiyo iliwafungia wanariadha wake kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya Rio 2016 na mashindano ya mwaka huu y ubingwa wa dunia mjini London.

Tangazo la IAAF lilifuata tangazo la Shirika la Kimataifa la Kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu – WADA mnamo Novemba 16 kuwa Urusi bado haitekelezi sharia za kimataifa kuhusu matzumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Rais wa Urusi Vladmir Putin aliituhumu Marekani kwa kuiwekea shinikizo Kamati ya IOC kuizuia Urusi kushiriki katika michezo ijayo ya Olimpiki ya msimu wa barafu mjini  Pyeongchang, Korea Kusini

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu