1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Internacional ya Brazil ni klabu bingwa ya dunia.

18 Desemba 2006

Ujerumani yachagua wanaspoti wake wa mwaka huku Internacional ya BRAZIL IKIIKOMEA fcbARCELONA;MABINGWA WA uLAYA !.= NA KUTAWAZWA KLABU BINGWA YA DUNIA:

https://p.dw.com/p/CHcr
bREMEN MABINGWA NUSU-MSIMU
bREMEN MABINGWA NUSU-MSIMUPicha: picture alliance /dpa

Jana Ujerumani ilichagua wanaspoti wake bora wa mwaka na timu ya taifa ya Ujerumani iliomaliza nafasi ya 3 nyuma ya mabingwa wa dunia-Itali na Ufaransa, imeibuka timu bora kabisa ya mwaka nchini.

Kwani, timu hii ilioongozwa na kocha Jürgen klinsmann ilitolewa tu na Itali katika nusu-finali baada ya kurefushwa mchezo.Timu hii ya ujerumani ilinyakua kura 4,165 ilizipiku timu nyengine zote za michezo mwaka huu nchini.

Michael Greis alieshinda medali 3 za dhahabu katika mchezo wa „biathlon“ katika michezo ya olimpik mjini Turin,Itali alichaguliwa „mwanaspoti wa mwaka“ wa kiume.

Greis alimpiku dereva mashuhuri Michael Schumacher stadi wa mbio za magari za Formula One.Kati Wilhelm alienyakua medali za dhahabu na fedha katika „biathlon“ huko Turin alichaguliwa mwanaspoti wa kike wa mwaka.

Katika Bundesliga:Werder Bremen iliikandika jana VFL Wolfsburg mabao 2-1 na kuibuka mabingwa wa nusu-msimu.

„2006 tumeonesha dimba barabara na ni kwa haki ni mabingwa wa nusu-msimu kileleni.Tunataka kuwa mabingwa na hii ndio shabaha yetu tangu mwanzo wa msimu huu na tunapania hata kutia fora katika kombe la Ulaya la UEFA.“-alinukuliwa mchezajhi mmoja wa bremnen kusema.

Mabingwa watetetezi Bayern Munich wananyatia nyuma nafasi ya 3 lakini wanajiwinda kwa changamoto ya jumatano ya kutetea taji lao la kombe la shirikisho la Ujerumani-DFB Pokale- kati yao na Alemaania Aaachen.

Kocha wa FC Barcelona ya Spain-mabingwa wa Ulaya,

Frank Rijkaard amedai leo kwamba mabingwa hao watarudi kutia fora licha ya kulazwa jana katika finali ya kombe la klabu bingwa za dunia na Internacional ya Brazil kwa bao 1:0.

Barceloona iliopigiwa upatu kuwika kwa kweli ilitamba katika hatua za kwanza za finali hiyo mjini Tokyo.Rijkaard hatahivyo, ameungama timu yake haijajiandaa barabara kwa changamoto hiyo.

Mabinbgwa wa Afrika-al Ahly ya Misri ilimaliza 3 nyuma ya Internacional na FC Barcelona.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza-uongozi wa Manchester United umepunguzwa kileleni kutoka pointi 8 hadi 2 mnamo muda wa juma moja.Kwani, Manchester ilinaswa na mtego wa panya wa West ham United na hilo likawa pigo la pili mnamo juma moja. Bao la West Ham lilitiwa dakika ya 75 ya mchezo na Nigel Reo-cocker.