1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

INSTANBUL:Waziri Steinmeier yupo nchini Uturuki akiwa njiani kuelekea Lebanon

7 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEe

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank Walter Steinmeier leo anatazamiwa kuwasili nchini Lebanon kutokea Uturuki ambapo anafanya ziara fupi.

Waziri Steinmeier anaeongozana na maafisa wa ushuru pamoja na walinzi wa mipaka amekaribisha uamuzi wa Uturuki wa kushiriki katika jukumu la kulinda amani nchini Lebanon.

Waziri Steinmeier amesema hayo baada ya kukutana na waziri mwanzake wa Uturuki Abdullah Gül.

Waziri huyo pia amewaambia wandishi habari kuwa wajerumani watasaidia katika taratibu za usalama wa abiria na mizigo kwenye uwanja wa ndege wa Beirut. Lengo la zoezi hilo ni kupunguza hatari ya silaha kupenyezwa kwa siri kutoka nje kwa ajili ya wapiganaji wa Hezbollah