MichezoIndonesia
Indonesia yawashtaki waliosababisha vifo vya watu 135
16 Januari 2023Matangazo
Polisi walifyetua gesi ya kutowa machozi ndani ya uwanja huo baada ya mashabiki kufurika uwanjani kufuatia kushindwa kwa timu ya Arema FC na mpinzani wake Persebaya Surabaya katika mechi ya nyumbani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23. Hatua hiyo ilisababisha tukio baya kabisa katika historia ya michezo duniani la mkanyagano mnamo mwezi Oktoba mosi mwaka jana. Rais wa nchi hiyo Joko Widodo aliunda tume ya uchunguzi wa tukio hilo ambayo imetoa tathmini yake kwamba gesi ya kutowa machozi ndio chanzo kilichosababisha msongamano wa mashabiki.