India: Rahul Gandhi apoteza kiti chake cha Bunge
25 Julai 2023Hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya mahakama kumtia hatiani mwanasiasa huyo wa upinzani Rahul Gandhi kutokana na kutoa matamshi yaliyopokelewa kama ni kumtusi Waziri Mkuu Narendra Modi.
Mwanasiasa Rahul Gandhi kiongozi wa chama cha upinzani cha Congress, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili lakini akaachiliwa kwa dhamana huku mawakili wake wakisema watakata rufaa kupinga hukumu ya siku ya Alhamisi iliyotolewa dhidi ya mteja wao. Hata hivyo, hukumu hiyo imemfanya mwanasiasa huyo Gandhi kuwa hastahili kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge kwa mujibu wa notisi kutoka kwa katibu wa bunge.
Gandhi alitoa maneno hayo wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita ambao chama tawala cha Hindu-nationalist Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu Narendra Modi kiliibuka mshindi. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanachama wa chama tawala cha Modi anayeitwa Purnesh Modi, ambaye alizingatia maoni ambayo Gandhi aliyatoa kwenye hotuba yake yam waka 2019 alipowataja wafanyabiashara wawili waliotoroka nchini, ambao wote wawili wana majina ya Modi. Na hapo Gandhi alisikika akiuliza "Inakuwaje wezi wote wana majina ya Modi?"
Soma:Kiongozi wa upinzani ahukumiwa kifungo cha miaka 2 India
Hakimu aliyetoa hukumu alisema kifungo cha miaka miwili jela kilikuwa halali kwa sababu kutoa hukumu nyepesi kwa mtuhumiwa kungetoa ujumbe usio sawa kwa watu". Kiongozi wa chama cha Upinzani cha Congress cha nchini India Mallikarjun Kharge amesema
Gandhi, mwenye umri wa miaka 52, ndiye kiongozi mkuu wa chama cha Congress, kilichowahi kuwa na nguvu kubwa ya siasa nchini India, na kinachojivunia juu ya kuukomesha utawala wa mkoloni Uingereza, lakini sasa kimebaki kuwa kivuli cha uwezo wake wa zamani. Rahul Gadhi ni mzaliwa katika nasaba maarufu ya kisiasa ya India ni mwana, ni mjukuu na kitukuu cha mawaziri wakuu wa zamani, kuanzia kiongozi wa uhuru wa India Jawaharlal Nehru.
Katika siasa za sasa za nchini India anajitahidi lakini si rahisi kuushinda ushawishi mkubwa wa Narendra Modi kwa wapiga kura Wahindu walio wengi nchini India.
Hukumu hiyo iliyotolewa jana Alhamisi ni baada ya miezi miwili tangu Rahul Gandhi alipohitimisha matembezi ya kuzunguka nchini kote ya kilomita 4,000 kutoka kwenye ncha ya kusini ya India hadi katika jimbo la Kashmir kwenye milima ya Himalaya katika jitihada za kukifufua chama chake na kujenga sura mpya katika kile alichokiita Bharat Jodo Yatra, kwa maana Tuungane katika mwendo wa kuisogeza mbele India.
Vyanzo: AFP/RTRE