Imran Khan na mkewe washtakiwa kwa ufisadi
27 Februari 2024Chama cha Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan kimesema Mahakama moja nchini humo imemshitaki Khan aliyekorokoroni pamoja na mkewe Bushra Bibi kwa madai ya kupokea kiwanja kama hongo wakati wa uongozi wake. Wote wawili wamekanusha mashitaka hayo.
Khan aliye na miaka 71 amefungwa jela tangu mwezi Agosti kwa madai ya mengine aliyoyakanusha. Tayari alishashitakiwa kwa madai mengine ya ufisasi yaliyompiga marufuku ya kushiriki katika masuala yoyote ya kisiasa Pakistan kwa muda wa miaka 10.
Wagombea wallioungwa mkono na chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni walishinda viti vingi bungeni lakini vyama vya upinzani vilivyoongozwa na Nawaz Sharif na Bhutto viliungana pamoja kuunda serikali ya mseto.