23 Aprili 2018
Matangazo
Sera hiyo mpya pia inalenga kulitafutia ufumbuzi tatizo kuhusu jinsi mataifa tajiri yaliyostawi kiuchumi duniani yanavyochangia kusababisha rushwa katika nchi zinazoendelea, kwa kushindwa kuzuia hongo na utakatishaji fedha au kuruhusu umiliki wa makampuni na watu wasiojulikana. Je, sera hii inatekelezeka? Na je shirika la IMF kweli lina uwezo wa kuyabana mataifa makubwa? Haya ni miongoni mwa maswali ambayo Josephat Chari alimuuliza Profesa wa uchumi Honnest Prosper Ngowi, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Kwanza alitaka kujua mtazamo wake kuhusu sera hii mpya. Unaweza kusikiliza mahojiano hapo chini.