1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF yaidhinisha mkopo wa $1 bilioni kwa Uganda

Yusra Buwayhid
29 Juni 2021

Bodi ya Shirika la Fedha Duniani, IMF imeidhinisha mkopo wa miaka mitatu wa dola bilioni 1 kuisaidia Uganda kujikwamua kwenye mgororo wa kiuchumi uliosababishwa na janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3vkaH
Yoweri Museveni
Picha: picture-alliance/dpa/A. Novoderezhkin

Msaada huo utairuhusu Uganda kupata mara moja dola milioni 258 kufidia matumizi ya serikali. Mwaka jana Uganda pia ilichukua mkono wa dharura wa takriban dola milioni 500 kulingana na taarifa za shirika hilo la IMF.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Tao Zhang amesema uchumi wa Uganda umeathiriwa sana na janga la ugonjwa wa COVID-19 lilopiga ulimwenguni kote, na kurejesha nyuma hatua nyingi zilizopigwa nchini humo kupunguza kiwango cha umaskini.

Ameongeza kwamba serikali ya Uganda itajitahidi kushughulikia kupunguza deni na kuwekeza katika sekta ya miundombinu, huku ikiongeza matumizi katika mchakato wa kutoa chanjo na kupunguza umaskini.