1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

IMF: Mabadiliko ya tabia nchi huenda yakaongeza vifo

30 Agosti 2023

Shirika la Fedha Duniani IMF linasema mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha mizozo katika mataifa yaliyo na hali tete kote duniani na yanachangia katika ongezeko la vifo.

https://p.dw.com/p/4Vm3z
IWF Logo, Schild
Picha: Maksym Yemelyanov/Zoonar/picture alliance

Katika ripoti yake iliyochapishwa leo, IMF inasema matukio ya kimazingira tu hayawezi kuchocheamizozo ila yanaweza kufanya hali zinazojitokeza kwenye mizozo kama njaa, umaskini na watu kuachwa bila makao, kuwa mbaya zaidi.

Ripoti hiyo inasema ifikapo mwaka 2060, vifo vinavyotokana na mizozo huenda vikaongezeka kwa asilimia 8.5.

Soma pia:Wanasayansi wajadili zaidi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, nchi ambazo zitaathirika zaidi ni zile zinazokabiliwa na mizozo na hali tete na huenda vifo vikaongezeka kwa hadi asilimia 14 katika mataifa yanayokabiliwa na ongezeko la joto.

Shirika hilo la fedha duniani limeonya kuwa, watu milioni 50 zaidi katika nchi hizo huenda wakakabiliwa na njaa kutokana na uzalishaji mdogo wa chakula.