Idadi ya waumini waliojiuwa kwa kukaa njaa Kenya yafikia 90
26 Aprili 2023Matangazo
Polisi wamesema wamesitisha zoezi la utafutaji wa miili zaidi kwa sababu hakuna nfasi kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti.
Watu hao waliamini kwamba wangeenda mbinguni iwapo wangefunga hadi kufa.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kithure Kindiki amesema mwanzilishi wa kanisa la Good News International Paul Mackenzie anastahili kufungwa jela maisha.
Shirika la msaada la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema watu zaidi ya 200 hawajulikani walipo.
Polisi wameeleza kuwa uchimbaji wa makaburi mengine zaidi unaendelea. Kiongozi wa kanisa hilo, mchungaji Paul Mackenzie amekamatwa akisubiri kufikishwa mahakamani.