1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndia

Idadi ya watu India kuipiku China katikati ya mwaka huu: UN

19 Aprili 2023

Makadirio ya Umoja wa Mataifa yaliyochapishwa yanaonyesha kuwa ifikapo katikati ya mwaka huu, India itakuwa nchi ya kwanza kwa idadi ya watu duniani, ikiipita China kwa takribani watu milioni tatu

https://p.dw.com/p/4QHbY
Indien | Weltbevölkerung
Picha: Kabir Jhangiani/ZUMA Press/picture alliance

Ripoti ya hali ya dunia ya Fuko la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya idadi ya watu, UNFPA inasema India itakuwa na watu bilioni 1, milioni 426 na laki nane (1.4286 bilioni) huku idadi ya watu wa China ikiwa bilioni 1, milioni 425 na laki saba (1.4257 bilioni).

Takwimu rasmi zinabainisha kuwa idadi ya watu wa China ilipungua mwaka jana, hiyo ikiwa mara ya kwanza kwa miongo sita.

Mbali na India na China, ripoti hiyo ya UNFPA imekadiria kuwa idadi jumla ya watu dunia itafikia bilioni nane na milioni 45 (8.045 bilioni) ifikapo katikati mwa mwaka huu wa 2023.