1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wasiokua na ajira imepungua kwa mwezi wa tatu mfululizo nchini Ujerumani

1 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF8E

Nürnberg:

Licha ya kuimarika soko la ajira msimu huu wa kiangazi,bado lakini hakuna dalili za kupunguaa kwa idadi kubwa watu wasiokua na kazi humu nchini.Ofisi kuu ya kazi imesema katika ripoti yake mjini Nürenberg,katika kipindi cha mwezi May uliopita watu milioni nne na laki nane na elfu sabaa wameandikishwa hawana kazi- Idadi hiyo imepungua watu laki moja na 61 elfu,ikilinganishwa na takwimu za mwezi wa April mwaka huu.Mkuu wa ofisi kuu ya kazi,Frank –Jürgen Weise anasema kazi za msimu wa kiangazi ndio chanzo cha kupungua idadi ya wasiokua na kazi.Waziri wa uchumi Wolfgang Clement amezungumzia juu ya matunda ya mageuzi yanayoanza kuchomoza.Upande wa upinzani unailaumu serikali ya muungano ya SPDF na walinzi wa mazingira,kuachilia mbali juhudi za kupambana na ukosefu ajira.