1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa kwa Corona yafikia 722 China

8 Februari 2020

idadi ya walokufa kwa maambukizi ya virusi vikali vya Corona nchini China yafikia 722 huku idadi ya waliombakuziwa nayo ikiongezeka kwa kasi na kupindukia 34,500.

https://p.dw.com/p/3XRxA
China Wuhan provisorisches Krankenhaus für Coronavirus-Patienten
Picha: picture-alliance/AP/Chinatopix

Idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya mripuko wa virusi vya corona imeongezeka na kufikia watu 722, ikipindukia rekodi ya vifo vilivyotokana na mripuko mwingine wa virusi vinavyofanana na hivyo vya SARS ambavyo viliikumba China Bara na Hong Kong miongo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa kamisheni ya afya ya taifa idadi nyingine ya watu 86 imepoteza maisha ambapo watano miongoni mwa hao wanatokea katika jimbo la Hubei, ambalo mripuko huko ulizuka Desemba. Kwa rekodi za kila siku kamisheni hiyo pia imesema visa 3,399 vimeripotiwa. Kwa hivi sasa zaidi ya watu 34,546 wameambukizwa virusi vyacoronakwa nchi nzima. Katika kipindi cha mwaka 2002 na 2003, ugonjwa wenye kufanana na huu unaosababaishwa na corona uliopewa jina la SARS ulisababisha vifo vya watu 650.

Japan Yokohama Kreuzfahrtschiff Princess Diamond mit Corona-Kranken
Meli ya starehe ya Princess Diamond ya Yokohama JapanPicha: picture-alliance/Xinhua/Du Xiaoyi

Meli ya starehe imeendelea kuwa kitisho

Meli ya starehe ya Japan Princess Diamond imekuwa ikiangaziwa zaidi katika kipindi hiki ambapo pia imeripotiwa visa vitatu vipya na kufanya jumla ya abiria wake 64 kuwekwa katika uangalizi maalumu kwa siku 14. Meli hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 3,700. Ijumaa Rais Xi Jinping wa China alizungumza na Rais Donald Trump na kuitaka Marekani kushiriki haraka katika kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona, na hasa kutokana na malalamiko ya baadhi ya nchi kuwazuia wasafiri kutoka China.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema abiria wa kigeni katika meli nyingine ya starehe iitwayo Holland America's Westerdam,hawatoruhisiwa kuingia Japan. Anasema watu wenye virusi wanahisiwa kuwa katika meli hiyo. Meli hiyo yenye jumla ya watu 2,000 ipo karibu na mji wa Okinawa na inatafuta namna ya kuweka nanga katika bandari nyingine.

Hata hivyo Marekani imetanagaza kutumia dola milioni 100 kuisaidia China na Mataifa mengine kukabiliana na mripuko huo. Tani 18 ya vifaa vimetolewa pia ikiwa msaada kutoka kwa watu wa Marekani. Miongoni mwa hivyo vimo vya kujikinga na maambukizi na vinginevyo. Mamia ya Wamerekani wameondolewa katika maeneo hatarishi.