1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa Afrika Kusini kufuatia mafuriko yapanda

13 Aprili 2022

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo Afrika Kusini imeongezeka na kufikia watu 59. Hali hiyo imesababishwa na mvua kubwa katika mji wa Durban na maeneo ya jirani ya mkoa wa Kwazulu Natal.

https://p.dw.com/p/49tjD
BG Südafrika | Erdrutsch Überflutung
Picha: ROGAN WARD/REUTERS

Taarifa ya mamlaka ya mji wa Durban imesema mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa makaazi na miundombinu kutoka maeneo ya vijijini, vitongoji hadi maeneo ya kifahari. 

Mvua zilizonyesha kwa siku kadhaa zimesababisha maeneo kufurika, kubomoa nyumba na kuharibu miundombinu huku maporomoko ya ardhi yakilazimisha huduma za treni kusitishwa. 

Idara ya kudhibiti majanga katika jimbo la KwaZulu-Natal, imewataka watu kusalia majumbani mwao na kuamuru wale wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhamia maeneo yenye muinuko.