1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo vya wanajeshi wa Marekani Iraq imepanda

Kalyango Siraj24 Machi 2008

Wanajeshi 4,000 wa Marekani ndio wameuliwa Iraq kuafikia sasa

https://p.dw.com/p/DTSx
Rais Bush, kushoto, akikutana na vikosi vya Marekani katika kambi ya Al-Asad katika mkoa wa Anbar , Iraq, Sept. 3, 2007. Rais wakati huo alifanya ziara ambayo haikutangazwa nchini Iraq. Idadi ya wanajeshi waliokufa hadi sasa ni 4,000Picha: AP

Idadi ya wanajeshi wa Marekani ambao wameuawa nchini Iraq kwa kipindi cha miaka mitano ya mgogoro huo imefika wanajeshi elf 4,baada ya wanajeshi wengine wanne kuawa katika shambulio la bomu mjini Baghdad.

Wanajeshi wanne wa Marekani wameuawa kusini mwa mji wa Baghdad,wakati gari walimokuwa wakisafiria wakifanya doria kulipuliwa na bomu ambalo lilikuwa limetegwa kando mwa barabara.

Vifo vya wanajeshi hayo,vinajumulisha wanajeshi wa Marekani ambao wameuawa katika mgorogoro huo kufikia 4,000.Hii ni kwa mujibu wa shirika la habri la AFP ambalo hesabu zake zimetegemea mtandao wa kujitegemea wa shirika la kufuatilia wahanga wa Iraq unaojulikana kama icasualities.org.

Taarifa ya kijeshi imeongeza kuwa mwanajeshi mwingine alijeruhiwa katika kisa hicho.

Mgogoro huo,ulioanzishwa na Marekani ilipoivamia Iraq mwaka wa 2003 sasa umeingia mwaka wake wa sita na pia umesababisha wanajeshi wa Marekani takriban 29,000 kujeruhiwa,kwa kujibu wa shirika la linalochunguza wahanga wa Iraq.

Asili mia 97 ya vifo vya wanajeshi hao ilitokea wakati rais Bush wa Marekani alipotangaza Mei mosi mwaka wa 2003 kuwa vita kamili vimekwisha.Wanajeshi wa Marekani baade walikumbana na vita vikali kati yao na wapiganaji wa chini kwa chini.

Mbali na hasara ya wanajeshi hao,katika mkesha wa kuadhimisha miaka mitano nchini Iraq,rais Bush alitetea uamuzi wake wa kuivamia Iraq,akiapa kutorudi nyuma akiahidi kuwa wanajeshi wa Marekani watamshinda adui,licha ya hasara inayopatikana ya vifa pamoja na wanajeshi.

Msemaji wa jeshi la Marekani mjini Baghdad,Rear Admiral Gregory Smith,amesema kifo cha kila mwanajeshi ni cha kusikitisha.

Huku idadi ya wanajeshi wa Marekani ambao wameuawa katika mgogoro wa miaka mitano ikifiakia idadi hiyo ,lakini wanajeshi wa Iraq wenyewe waliopoteza maisha yao katika mgogoro huo idadi yao ni mara tatu zaidi ya wanajeshi wa Marekani.Tena idadi ya raia wa kawaida inakadiriwa kuwa zaidi ya elf 10 au zaidi.

Shirika moja ambalo linafuatilia majeruhi nchini Iraq likitumia ripoti ambazo zinachapishwa, kupitia wavuti wake, icasualties.org,linaonyesha kama wanajeshi wa Iraq takriban 8,000 wameuawa tangu uvamizi wa mwezi machi mwaka wa 2003.Lakini mwaka jana serikali ya Iraq ilitoa idadi ya wanajeshi wa Iraq waliouawa kama wanaofikia 12,000.

Miito imeanza kusikika Marekani ikitaka wanajeshi wake kuondolewe kutoka Iraq kutokana na vifo vyao kuwa vingi.

Suala hilo limejitokeza katika kampeini za urais nchini Marekani.Wanaogombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic,Hillary Clinton na Baraka Obama wanataka majeshi yaondolewe kutoka Iraq.

Vita vilivyoiletea hasara kubwa Marekani,mbali na vita vikuu vya vya dunia vya mara mbili, ni vita vya Vietnam.Wanajeshi 58,000 waliuawa kati ya mwaka wa 1964 na 1973.Hii ikiwa na maana ya mwanajeshi mmoja alikuwa akiuliwa kwa wastani wa kila siku.

Kwa wastani ni wanajeshi wawili ndio hufariki kila siku nchini Iraq.

Katika mwaka wa kwanza wa 2003 wanajeshi wa Marekani waliouawa ni 846,mwaka wa 2004 wanajeshi 849, mwaka wa 2005 wanajeshi 846 na mwaka wa 2006 wanajeshi 822.

Na tangu mwaka huu wanajeshi 96 wa Marekani ndio wameuawa.