Idadi ndogo ya Watoto kuimarisha Uchumi
20 Novemba 2014Ripoti hiyo mpya inasema jumla ya mataifa 59 yapo katika kitisho cha gawio la idadi ya watu, ambapo umri wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi inaongezeka kutokana na kupungua kwa idadi ya vifo.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye kuhusika na idadi ya watu limesema mataifa hayo yote mengi ya hayo yakiwa Afrika yangalifuata mfano wa uchumi wa Asia Mashariki, kama Korea Kusini ambayo ukuaji wake tangu miaka ya 70 ulitokana na idadi ya watu.
Miujiza ya kiuchumi ambayo imeshuhudiwa Asia Mashariki inaweza kujidhihirishwa kwa mataifa mengi masikini kwa hivi sasa.
Ripoti hiyo inasema vilevile kuna thibitisho linalopendekeza gawio la idadi ya watu lingaliweza kufanya zaidi katika namna ya mfumo wa kidemokrasia.
Ripoti imebaini kwamba gawio kwa vijana liliongezeka katika miaka ya 2010 na kuanza kupungua ikiwa na maana watu wenye umri wa kufanya kazi katika mataifa hayo yote itaongezeka zaidi ya mara mbili ifikapo 2050.
Ukizingatiwa mfano wa taifa la Nigeria, taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Africa wimbi la ongezeko la idadi ya watu litasaidia kuongeza pato la ndani endapo litasaidiwa na sera nzuri na uwekezaji.
Uwekezaji huo ikimaanishwa elimu, na hasa kwa wasichana. Wasichana lazima waende shule alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Babatunde Osotimehin pale alipozungumza na shirika la habari la AFP katika mahojiano maalumu.
Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kusema huduma ya afya na hasa ya afya ya uzazi lazima ipatikane ili wanawake waweze kufanya uamuzi kwa maisha yao.
Lakini mmoja kati ya madaktari wazuri nchini Nigeria ameonya kwamba sekta ya afya katika mataifa yaliyokumbwa na Ebola ipo katika wakati mgumu na kwamba itaathiri wanawake wajawazito na watoto.
Dokta huyo anasema Kunaweza kutokea vifo vingi pengine hata kuzidi ilivyo katika Ebola.
Ripoti hiyo ilisema serikali inapaswa kuwa tayari kuchukua faida ya gawio la idadi ya watu kama nafasi ya mara moja kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa haraka.
Aliongeza kuwa Bila mfumo imara wa kiuchumi na kuiunga mkono sera hiyo , mgao wa idadi ya watu hauwezi kuwa barabara kamilifu.
Aidha Nchi zilizotajwa katika ripoti hiyo ni pamoja na baadhi ya mataifa kutoka mabara mengine nje ya Afrika kama Afghanistan, Iraq, Papua New Guinea na Yemen.
Ripoti ilisema kuwa nchi zote zilikuwa katika njia ya mpito katika suala la idadi ya watu ambazo zilianza kupungua vifo vya watoto wachanga, ambayo kwa upande zilitoa wito kwa wazazi kuwa na watoto wachache na kuwekeza zaidi katika elimu yao na afya.
Kimsingi,wanawake katika mataifa yanayoendelea wanazaa watoto zaidi ya matakwa yao. Na hawapati njia za kisasa za uzazi wa mpango.
Mtalaamu Osotimehin anasema hivi sasa kuna zaidi ya wanawake million 220,wenye kuhitaji uzazi wa mpango na kwamba hawapati huduma hiyo.
Ripoti hii imezingatia utafiti uliofanyika katika maeneo ya Asia Mashariki kama China,Hong Kong,Japan, Korea Kusini na Singapore
Mwandishi:Nyamiti Kayora/AFP
Mhariri:Mohamed Abdul Rahman