1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iceland kucheza dimba la Ulaya kwa mara ya kwanza

7 Septemba 2015

Iceland kisiwa chenye wakaazi 330,000 pia taifa lenye idadi ndogo kabisa ya wakaazi kufuzu katika mashindano hayo ya ubingwa wa Ulaya, baada ya kutoka sare bila kufungana na Kazakhstan

https://p.dw.com/p/1GSLw
UEFA Euro 2016 Qualifikation Island vs Kasachstan
Wachezaji wa Iceland wakipongezeanaPicha: picture-alliance/epa

Ilikuwa ikihitaji pointi moja tu kuchukuwa uongozi wa kundi A. England ilikuwa ya kwanza kufuzu kuingia kinyanganyiro hicho cha mataifa 24, mashindano yatakayofanyika nchini Ufaransa . England iliimwagia mvua ya magoli San Marino na kuondoka na ushindi wa mabao 6-0.

Fußball San Marino England EM-Qualifikation Wayne Rooney
Rooney akisherehekea bao lakePicha: Reuters/C. Recine

Wakati huo huo mshambuliaji wake Wayne Rooney amesawazisha rekodi ya Bobby Charlton alipofunga bao la 49 akiwa na timu ya taifa ,bao la mkwaju wa penalty lililofungua mvua hiyo ya magoli dhidi ya San Marino .Rooney anapanga kuvunja rekodi hiyo katika pambano dhidi ya Uswisi Jumanne ijayo kwenye uwanja wa Wembley.Jamhuri ya Cheki ikaibwaga Latvia 2-0, wakati Uholanzi ilipata pigo isilolitarajia , ilipokandikwa na Uturuki mabao 3-0 na sasa inakabiliwa na kitisho cha kutofanikiwa kucheza mashindano ya ubingwa wa Ulaya

Matokeo ya mechi nyengine, Bosnia iliitandika Andorra 3-0, Ubeligiji ikaibwaga Cyprus bao moja kwa bila, Italia ikaifunga Bulgaria bao 1-0 na sasa ina pointi mbili zaidi ya Norway iliofanikiwa kuitandika Croatia 2-0 . wales inasubiri mechi zilizobaki kuamua ikiwa itafanikiwa kwa mara ya kwanza kucheza fainali za ubingwa wa ulaya tangu iliposhiriki katika kombe la dunia 1958. Wales ilitoka sare jana na Israel bila kufungana mjini Cardiff.

Barani Afrika michuano ya kuwania nafasi ya kufuzu kwa ajili ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika ilifanyika mwishoni mwa juma, ambapo watetezi wa kombe hilo Cote d´Ivoire chini ya kocha mpya Michel Dussuyer walilazimishwa sare ya bila kwa bila na Sierra Leone, wakati washindi wa zamani , Algeria, Cameroon, misri na Zambia zote ziliibuka na ushindi. Algeria iliibwaga Lesotho 3-1, Cameroon iliochuana na Gambia mjini Banjul, ikarudi nyumbani na ushindi wa bao 1-0. Misri iliokosa kushiriki fainali za kombe tatu zilizopita za kombe la mataifa ya Afrika ikaibwaga Chad mabao 5-1 huku Basserm Morsi akiuona wavu mara tatu. Zambia ikailazimisha Kenya isalimu amri ilipoipa kipigo cha mabao 2-1 .

Ama Mauritania iliishtuwa Afrika kusini Jumamosi ilipoifunga mabao 3-1 na kuongoza kundi lake kwa muda hadi Cameroon iliporudi kileleni hapo jana baada ya kuibwaga Gambia. Makosa ya mlinda lango na nahodha wa Bafana bafana Itumeleng Khune dakika tano baada ya mchezo kuanza mjini Nouakchott yaliipa bao la kwanza Mauritania . Pia Siyabonga zulu alipewa kadi nyekundu na muamuzi baada ya kipindi cha mapumziko akiiacha timu yake na wachezaji 10.

Fußball WM 2010 Fans Flash-Galerie
mashabiki wa bafana bafana wakipigwa na bunbuwaziPicha: AP

Ghana ikiitandika Rwanda bao 1-0.Tanzania ilitoka sare katika uwanja wa nyumbani mjini Dar es salaam na Nigeria bila kufungana .Akizungumza na DW,mwalimu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa alisema ameyapokea vizuri matokeo hayo na anafurahi kuona vijana wake wanajituma, akitumai kwamba hata kama hawatafuzu lakini Tanzania itaweza kuwa na timu nzuri kabisa katika kipindi cha miaka michache ijayo. Uganda iliotoka sare mchezo uliopita dhidi ya Tanzania, iliilaza Comoro 1-0 , baada ya Rais Yoweri Museveni kuamua kuilipia gharam za usafiri akitoa euro 190,000 . Bao hilo pekee lilifungwa mnamo kipindi cha kwanza na Tonny Mawejje anayecheza kandanda la kulipwa nchini Iceland.

Shirikisho la kandanda la kimataifa FIFA limetoa orodha mpya ya mtazamo wa timu bora za taifa duniani.Chile, mabingwa wa kombe la Amerika-Copa America- sasa imepanda nafasi mbili juu hadi nafasi ya 8, wakati Argentina ikiendelea kubakia nafasi ya kwanza . Chile imechukua nafasi ya England ambayo imeshuka hadi nafasi ya 10. Ubeligiji imeipiku Ujerumani ikishika nafasi yake ya pili na kuiacha ikiwa ya tatu, Colombia iko nafasi ya nne na Brazil ya tano. Kwa upande wa nchi za kiafrika, inayoongoza ni Algeria ikishika nafasi ya 19 katika orodha ya dunia. Kwa upande wa mataifa ya Amerika kati na eneo la Caribbean Mexico inaongoza kanda hiyo ikiwa nafasi ya 26 katika orodha jumla ya timu bora duniani wakati Iran ikiongoza kwa upande wa Asia ikiwa nafasi ya 40.

Katika ringi ya mabondia ,Muingereza Jamie Mc Donellel amelitetea taji lake la uzito wa bantam katika Shirika la ndondi la WBA baada ya kumshinda kwa pointi Mjapani Tomoki Kameda katika marudio ya pambano lao la mapema mwaka huu. Kameda alitarajia angeweza kulipiza kisasi baada ya kushindwa na McDonell kwa mara ya kwanza katika historia yake ya ndondi za kulipwa miezi sita tu iliopita. Kameda mwenye umri wa miaka 24 na bingwa wa zamani wa dunia mzaliwa wa Osaka alihamia Mexico akiwa na umri wa miaka 15 na wakati mmoja yeye na ndugu zake wawili wa kiume – wote walikuwa mabingwa wa dunia. Kwa upande wake ushindi wa McDonell dhidi ya Kameda ni wa 19 mfululizo.

Formel 1 Belgien Spa-Francorchamps Lewis Hamilton
Hamilton akisherehekea ushindiPicha: Getty Images/AFP/A. Isakovic

Katika ubingwa wa dunia wa mbio za magari, Muingereza Lewis Hamilton alishinda mbio za Grand Prix za Italia hapo jana na kuimarisha uongozi wake wa mashindano ya Formula One, akiwa b sasa na pointi 53.dereva wa mwenzake wa kikosi cha Mercedes na mpinzani wake wa karibu Nico Rosberg alilazimika kujitoa bada ya gari lake kukumbwa na matatizo. Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari alimaliza wapili.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, afp,rtr,dpa

Mhariri:Yusuf Saumu