Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imesema haitishiki na itaendelea kufanya kazi zake kwa uhuru na uwazi, ikiwa ni siku moja baada ya Mshauri wa Usalama wa Marekani, John Bolton, kutishia kuiwekea vikwazo mahakama hiyo endapo itachunguza kilichofanywa na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan. Papo kwa Papo 11 Septemba 2018.