1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA yatahadharisha juu ya hatari karibu na Zaporizhzhia

7 Mei 2023

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia ametahadharisha hatari inayoweza kutokea katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia wakati huu wa zoezi la kuwahamisha watu linapoendelea.

https://p.dw.com/p/4R0SX
Wien | IAEO | Rafael Mariano Grossi
Picha: Dean Calma/dpa/IAEA/picture alliance

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia Rafael Grossi, ametahadharisha kwamba hali katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine kinachodhibitiwa na Urusi inaweza kuwa ya hatari wakati huu ambapo zoezi la kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo yaliyo karibu na kituo hicho. Mkuu wa shirika la Kimataifa la kudhibiti nishati ya Atomiki, ametaka hatua zichukuliwe ili kuhakikisha usalama katika kituo hicho kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya wakati huu ambapo shughuli ya kuwahamisha watu inaendelea katika mji wa karibu na kituo hicho wa Enerhodar. Gavana aliyewekwa na Urusi katika sehemu ya mkoa wa Zaporizhzhia inayodhibitiwa na Urusi amesema mamalaka ya eneo hilo chini ya uongozi wake ndio iliyoamuru zoezi la kuwahamisha watu wanaoishi kwenye vijiji vilivyo karibu na kituo cha nyuklia kwa lengo la kuwanusuru na mashambulio ya makombora yaliyoongezeka kwenye eneo hilo katika siku za hivi karibuni.