1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

IAEA yaonya juu ya shughuli za kijeshi Zaporizhzhia

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA Rafael Grossi ameonya leo juu ya kuongezeka kwa shughuli za kijeshi katika maeneo yanayokizunguka kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia.

https://p.dw.com/p/4PRsa
Ukraine Saporischschja | Chef der IAEA Rafael Grossi besucht das AKW
Picha: RIA Novosti/SNA/IMAGO

Rafael Grossi ambaye amekitembelea kinu hicho ambacho ndicho kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, amesema kanuni hizo ni pamoja na kuweka ahadi za kutokishambulia. Wakati huo huo Ukraine imearifu kuwa imelishambulia ghala la vifaa vya ujenzi wa reli katika mji wa Melitopol unaodhibitiwa na Urusi, kukiwapo uvumi kuwa Ukraine inajiandaa kuvishambulia vikosi vya Urusi ilivyochoshwa na operesheni zilizoshindwa za kusonga mbele mnamo majira ya baridi.

Nayo Marekani imeiarifu Urusi kuwa itasitisha kabisa kubadilishana data za kinyuklia kama jibu kwa hatua ya Urusi ya kusimamisha makubaliano ya kupunguza mashindano ya kuunda silaha za nyuklia maarufu kama New Start.