1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA: Tani 2.5 za urani zimetoweka nchini Libya

16 Machi 2023

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia (IAEA) Rafael Grossi amesema takriban tani 2.5 za madini ya urani zimetoweka bila maelezo kwenye kituo kimoja nchini Libya.

https://p.dw.com/p/4OklJ
Director General of the International Atomic Energy Agency (IAEA), Rafael Mariano Grossi and Ukrainian Energy Minister German Galushchenko talk at South Ukraine Nuclear Power Plant
Picha: Nacho Doce/REUTERS

Grossi ametoa taarifa hiyo kwa nchi wanachama wa shirika hilo na kubaini kwamba wakaguzi waligundua siku ya Jumanne kuwa mapipa 10 yenye madini ya Urani hayakuwepo kama ilivyotajwa awali katika eneo hilo.

IAEA imesema itaendelea na uchunguzi ili kubaini mazingira ya uhamisho huo. Mwaka 2003, Libya iliachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia chini ya kiongozi wake wa muda mrefu Moamar Gaddafi.

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini imekuwa katika mzozo mkubwa wa kisiasa tangu kuangushwa kwa utawala wa Gaddafi mwaka 2011.